PADRE ALIYEWAVUA MABINTI BARAKOA NA KUWABUSU KANISANI AZUA GUMZO


PADRI huyo ambaye anasemekana kuwa wa Kanisa la Anglikana nchini Ghana, anaonyeshwa akiwa amevalia nguo za kijani, kisha aliwaita wanafuniz hao kwenye mimbari, akawavua barakoa zao kabla ya kuwabusu.

Kelele za kushangiliwa pia zinasikika kwenye kanisa hilo. Kisa hicho kinaripotiwa kutokea katika taasisi ya St Monica’s College of Education, Dayosisi ya Asante-Mampong.

Uchunguzi wafanywa

Kufuatia kuzagaa kwa video hiyo, uongozi wa Kanisa la Anglikana nchini Ghana, katika taarifa Jumatatu, Agosti 17,2021 umesema kwamba uchunguzi utaanzishwa kufuatia tukio hilo.
Mkuu wa dayosisi hiyo George Dawson-Ahmoah, pia alisema kanisa hilo litashughulikia namna wanafunzi hao watakavyopatiwa ushauri nasaha punde baada ya uchunguzi kukamilika.

“Kanisa limehuzunishwa na habari hizo na lingependa kusema uchunguzi umeanzishwa ghafla na padri huyo atachukuliwa hatua chini ya sheria na kanuni za Kanisa la Anglikana,” ilisoma taarifa hiyo.

Padri huyo aliyetambuliwa kwa jina, Obeng Larbi anadaiwa kuwabusu wanafunzi hao wa mwaka wa mwisho kama njia ya kuwashukuru kwa kujitolea kwa kusoma bibilia wakati wa ibada za kanisa hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post