Serikali Yawataka Wananchi Kutembea Vivutio Vya Utalii Nchini


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewataka Wananchi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini baadala ya kuona vivutio hivyo vipo kwa ajili ya wageni pekee

Ameyasema hayo  wakati alipokuwa akizungumza na Washiriki wa mashindano ya mbio za Utalii Marathon Arusha yaliyofanyika jana Jijini Arusha  yaliyolenga kuhamasisha Utalii wa ndani has katika kipindi cha ugonjwa wa UVIKO 19 uliotiokisa sekta ya utalii ulimwenguni

Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inahamasisha utalii wa ndani kupitia michezo mbalimbali ili wananchi waanze utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii tulivyojaliwa nao.

''Vivutio vya Utalii tulivyonanvyo ni vyetu sote tembeleeni muone uzuri na upekee wa vivutio vilivyopo nchini.

Katika hatu nyingine, Waziri Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa wadau wengine wa Utalii kuanzisha matukio MENGINE y a michezo itakayohamasisha watalii kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.


Amesema michezo imkuwa ikipendwa na watu mbalimbali ndani na nje ya nchi hali itakayosaidia kuchochea utamaduni wa watu mbalimbali kutembelea viv ui hivyo

Akizungumza wakati hafla hiyo ya utoaji wa zawadi kwa washindi Mbio za Mashindano, amesema ya utalii inataka kubadilsha  mtazamo ili watu wengi waweze kujifunza zaidi Dkt. Ndumbaro

 Dt, Ndumbaro aemezitaka sekta binafsi kuhakikisha zinawekeza hasa katika   kipindi hikiambachp sekta ya utalii nchii imetikiswa kwa kiasi kikubwa

Dkt, Ndumbaro  amesema watalii wa ndani  hususani sekta ya utalii ni watu muhimu sana kwa vile kazia binafsi ni kuchakata hoja na kutoa maoni





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments