NAIBU WAZIRI KASEKENYA AWASISITIZA WAKANDARASI NCHINI KUMALIZA MIRADI KWA WAKATI

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa kwanza), akikagua ujenzi wa daraja dogo la Mvugwe, katika barabara ya Kabingo, Kasulu hadi Manyovu (KM 260) mkoani Kigoma, kipande cha Mvugwe hadi Nduta (KM 59.35), kinachojengwa na Kampuni ya STECOL Corporation kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akimuelekeza jambo Mhandisi Mkazi Tadesse Dirba (Wakwanza kulia), wakati akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kabingo- Kasulu hadi Manyovu, kipande cha Kanyani hadi Mvugwe (KM 70.5), kinachojengwa na Kampuni ya Sinohydro Corporation Limited kwa kiwango cha lami .

Mhandisi Mkazi Khatibu Khamis, akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa tatu kushoto), wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kabingo, Kasulu hadi Manyovu (KM 260) mkoani Kigoma, kipande cha Mvugwe hadi Nduta (KM 59.35), kinachojengwa na Kampuni ya STECOL Corporation kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akimuelekeza jambo Mhandisi Mkazi Khatibu Khamis (wa pili kushoto), wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kabingo, Kasulu hadi Manyovu (KM 260) mkoani Kigoma, kipande cha Mvugwe hadi Nduta (KM 59.35), kinachojengwa na Kampuni ya STECOL Corporation kwa kiwango cha lami.

Mtaalamu wa kupima udongo katika maabara ya kampuni ya Zhejiang Communications Construction Group Co. Ltd (ZCCC), inayojenga kipande cha barabara ya Manyovu hadi Kasulu (KM68.25) mkoani Kigoma, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati), wakati akikagua utendaji kazi wa maabara hiyo. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza na wananchi wa eneo la Mvugwe mkoani Kigoma, baada ya kumaliza ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kabingo- Kasulu hadi Manyovu, kipande cha Kanyani hadi Mvugwe (KM 70.5), kinachojengwa na Kampuni ya Sinohydro Corporation Limited kwa kiwango cha lami.

Ujenzi wa daraja dogo la Mvugwe ukiendelea katika barabara ya Kabingo, Kasulu hadi Manyovu (KM 260) mkoani Kigoma, kipande cha Mvugwe hadi Nduta (KM 59.35), kinachojengwa na Kampuni ya STECOL Corporation kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akimuelekeza jambo Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, wakati akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kabingo, Kasulu hadi Manyovu, kipande cha Kanyani hadi Mvugwe (KM 70.5), kinachojengwa na Kampuni ya Sinohydro Corporation Limited kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza na Mhandisi Mkazi Gelawdiwos. kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Kabingo, Kasulu hadi Manyovu mkoani Kigoma, kipande cha Manyovu hadi Kasulu (KM68.25), kinachojengwa na Mkandarasi Zhejiang Communications Construction Group Co. Ltd (ZCCC), kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma.

PICHA NA WUU

.....................................................................................

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amewataka Wakandarasi wanaojenga miradi ya barabara nchini kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana hususan katika kipindi cha kiangazi ili kukamilisha miradi kwa wakati.

Kasekenya ameyasema hayo wilani Kasulu, mkoani Kigoma, wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi wa barabara ya Kabingo- Kasulu- Manyovu yenye urefu wa kilometa 260.

Amefafanua kuwa kitendo cha kuongeza muda wa kufanya kazi kwa Makandarasi hao kutafidia muda watakaoupoteza wakati wa kipindi cha masika ambapo miradi ya barabara husimama kutokana na mvua.

"Nimepita kuangalia maendeleo ya mradi huu wa barabara yenye urefu wa kilometa 260 ambao unatekelezwa na makandarasi mbalimbali katika vipande vinne tofauti, nimefurahishwa na baadhi ya makandarasi hawa kujiongeza kwa kuamua kuongeza muda wa ufanyaji kazi, hii itasaidia hata miradi kukamilika kwa wakati, hivyo nawaagiza makandarasi wengine nao kuiga mfano huu”, amesema Kasekenya.

Aidha, amewataka Makandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo kuzingatia viwango vya ubora wakati wa ujenzi wa miradi hiyo na kuhakikisha kuwa kila kilichoandikwa kwenye mchoro ndicho kinachofuatwa.

Amewasisitiza Makandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo kubainisha changamoto zozote zinazowakabili ili zitatuliwe mapema wakati mradi ukiwa kwenye hatua za awali.

Amewahakikishia Makandarasi hao na wasimamizi wake kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa wakati ili kuhakikisha miradi haikwami kutokana na ucheleweshaji wa malipo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kasekenya wakati akimalizia ziara yake wilayani Kibondo mkoani humo, akiwa anakagua kipande cha Tatu cha barabara cha Mvugwe - Nduta Junction (Km 59.35) amesema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza muda wa safari kutoka wilayani hapo kuelekea mikoa mingine kama vile Mwanza, Kagera na nchi jirani ya Burundi.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Afrisa, ambao ni wasimamizi wa kipande cha barabara kutoka Kanyani - Mvugwe (Km 70.5) Reginald Kaganga, amesema kuwa kipande hicho kinatekelezwa na Mkandarasi Sinohydro ambapo kazi zinazoendelea kwa sasa ni kusafisha, kujenga tuta na kuweka tabaka la mwanzo la barabara pamoja na ujenzi wa makalvati.

Nao wananchi wa Kasulu wamesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kutarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji wa mazao na hivyo kuweza kuyafikia kwa urahisi masoko ya ndani na nje ya nchi.

Barabara hii ya Kabingo- Kasulu- Manyovu yenye urefu wa kilometa 260 inajengwa kwa vipande vinne tofauti ambavyo ni Kasulu – Manyovu (Km 68.25), Kanyani – Mvugwe (Km 70.5), Mvugwe – Nduta Junction (Km 59.35) na Nduta Junction – Kabingo (Km 62.5) ambapo ujenzi wa vipande hivi vyote unafadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika ( AfDB).

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments