RUWASA YAANZA KUTEKELEZA KWA KISHINDO MIRADI YA MAJI BUDUHE NA KADOTO SHINYANGA


Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi (kulia) wakiangalia mabomba ya maji yakipakiwa tayari kusafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto.

***
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga imeanza kutekeleza miradi ya maji safi Buduhe kata ya Salawe na Kadoto kata ya Lyamidati katika katika halmashauri ya wilaya Shinyanga ambapo tayari imesafirisha mabomba ya kusambazajia maji ili kuhakikisha inatatua changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili wakazi zaidi ya 8,000 wa maeneo hayo.

Akizungumza leo Jumatano Julai 7,2021 wakati wa kusafirisha mabomba ya maji kutoka ofisi za RUWASA zilizopo Mjini Shinyanga kwenda kwenye maeneo ya miradi, Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi amesema utekelezaji wa miradi hiyo unaanza Julai 2021 hadi Oktoba 2021 ikigharimu jumla ya shilingi milioni 381.

Ameeleza kuwa miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga inatekelezwa na RUWASA ikitarajia kuwanufaisha wananchi zaidi ya 8,000 huku akisisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi.

“Tayari zoezi la kuchimba mitaro limeanza na haya ni mabomba ya maji kwa ajili ya mradi wa maji safi wa Buduhe kata ya Salawe ambao pia utanufaisha kijiji cha Nzoza ambao utakuwa na vituo 10 vya kuchotea maji (DP), ukiwa na mtandao wa bomba Kilomita 9.85 ukigharimu jumla ya shilingi milioni 195. Pia tunapeleka mabomba haya katika maradi wa maji safi wa Kadoto kata ya Lyamidati ambapo mtandao wake wa bomba ni kilomita 7.8 ukiwa na vituo vya kuchotea maji (DP) 6 ukigharimu jumla ya shilingi milioni 186”,amesema Nkopi.

Kwa upande, Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi ambaye ameshuhudia zoezi la kusafirisha mabomba ya maji kuelekea kwenye maeneo ya miradi ya maji amesema sasa wananchi wa Buduhe na Kadoto wategemee kupata huduma ya maji safi na kuondokana na tabia ya wizi wa maji kwa kutoboa mabomba ya maji kutoka Ziwa Victoria yaliyokuwa yanapita kwenye maeneo yao lakini wakawa hawapati huduma ya maji.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje amesema ni faraja kubwa kwa wakazi wa Kadoto na Buduhe kupata huduma ya maji ambayo imekuwa changamoto ya muda mrefu kwenye maeneo hayo licha ya bomba la maji kupita kwenye maeneo hayo.

“Maji hayana mbadala, tunafarijika sana kuona serikali inatatua kero za wananchi. Kupatikana kwa huduma ya maji katika maeneo haya itasaidia pia kuongeza uchumi kwani wananchi walikuwa wanatumia muda mwingi kufatuta huduma ya maji na kujikuta hawafanyi shughuli za maendeleo”,amesema Mboje.

Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi (kulia) wakiangalia mabomba ya maji yakipakiwa tayari kusafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kushoto) akimwelezea Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi kuhusu mabomba ya maji kwa ajili ya miradi ya maji safi ya Buduhe na Kadoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi mabomba ya maji kwa ajili ya miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi mabomba ya maji kwa ajili ya miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi akimuonesha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi akimuonesha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (wa katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon wakiangalia mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (wa pili kushoto) akifurahia jambo n Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (wa kwanza kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon wakati wakikagua mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi na wafanyakazi wa RUWASA wakiwa kwenye mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi akikagua mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments