RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MOROGORO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, June 15, 2021

RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MOROGORO

  Malunde       Tuesday, June 15, 2021


Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro, ambako Wafanyabiashara wadogo waliondolewa kwa nguvu hivi karibuni.
Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu kusimamia jambo hilo.

Amesema amesikitishwa na kitendo cha kuondolewa kwa nguvu kwa Wafanyabiashara hao, na kwamba kama ingekuwa ni lazima Wafanyabiashara hao kuondolewa ingetumika njia nyingine na si nguvu na kuharibu bidhaa zao.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza uamuzi huo mkoani Mwanza wakati wa mkutano wake na Vijana wa Tanzania kupitia vijana wa mkoa huo.

Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan,  Wafanyabiashara hao walitengewa eneo la mbali kwa ajili ya  kufanya biashara zao na walipoona hakuna biashara waliamua kurudi maeneo ya mjini na ndipo walipoanza kuondolewa kwa nguvu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post