RAIS SAMIA AMTEUAJAFFAR HANIU KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Jaffar Mohamed Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu).


Kabla ya uteuzi huo, Bw. Haniu alikuwa Mtendaji Mkuu wa vyombo vya habari vya Africa Media Group Limited.

Bw. Haniu anachukua nafasi ya Bw. Gerson Partinus Msigwa ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Uteuzi wa Bw. Haniu umeanza leo tarehe 09 Juni, 2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments