RAIS SAMIA ATOA AGIZO MAITI KUZUIWA MOCHWARI KISA DENI LA MATIBABU


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri wa Afya,  Dk Dorothy Gwajima kuweka mpango mzuri wa ndugu kulipa deni la hospitali ili ikitokea  mgonjwa wao amefariki dunia wakati akitibiwa, maiti isizuiwe.

Amesema utaratibu wa sasa ambao umekuwa ukizuia kutoa maiti hospitalini kwa kigezo cha kulipa gharama za matibabu kabla ya kifo si mzuri.

Rais Samià Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati wa mkutamo wake na Wanawake wa Tanzania kupitia Wanawake wa mkoa wa Dodoma.

Amesema ni vema wakati wa matibabu ndugu wa mgonjwa ama mgonjwa mwenyewe akawa anapatiwa gharama za matibabu za kila siku, badala ya kusubiri hadi kifo kinapotokea, na hivyo kuleta usumbufu.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments