WAKWAPUA POCHI WANASWA MOROGORO - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, June 1, 2021

WAKWAPUA POCHI WANASWA MOROGOROKamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu
***
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia vijana 34 kwa tuhuma za wizi wa kukwapua mali za wananchi kwa kutumia pikipiki ambapo jumla ya pikipiki nane zinashikiliwa na jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu, amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika maeneo ya Mtawala, Kidabaga, Mwembesongo na Mji Mpya Manispaa ya Morogoro, ambapo inadaiwa hutumia njia ya kupakizana vijana wawili kwenye pikipiki hizo na kuvizia watembea kwa miguu wanaoongea na simu au walioshika mikoba na kuikwapua.

Katika hatua nyingine SACP Musilimu, amesema jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ikiwemo vipande vya nyaya za shaba mpya na zilizounguzwa huku nyingine zikiwa zimefumuliwa kwenye 'transfomer' zenye jumla ya uzito wa kilogramu77.9 zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala la mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Ahmed lililopo mtaa wa Modeco Manispaa ya Morogoro.

Chanzo- EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages