BIBI WA MIAKA 72 ATESEKA NA MIMBA ALIYOBEBA MWAKA WA 30 SASA




 Bibi mmoja mwenye umri wa miaka 72 nchini Nigeria anakumbana na maisha magumu kutokana na hali yake isiyokuwa ya kawaida. Bibi huyo amekuwa "mjamzito" kwa zaidi ya miaka 30. 

Katika video iliyochapishwa kwenye Instagram na @kingtundeednut, bibi huyo anaonyeshwa na tumbo lake likiwa limechomoza akisimulia hali yake.

 Kulingana naye, haya yalianza miezi sita baada ya kumpoteza mume wake na alipofanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, aligunduliwa kuwa ana mimba ya mtoto wa kiume. 

Tatizo lilianza wakati alikwenda hospitalini miezi sita baadaye na kuambiwa kuwa kile alichobeba tumboni si mtoto. Madaktari walimuambia mama huyo ambaye aliwapoteza wanawe katika hali tatanishi kuwa njia moja pekee ya kuondoa uvimbe huo ni kupitia upasuaji ambao ni hatari.

Tangu siku hiyo bibi huyo amekuwa akiishi na matumaini kuwa siku moja kilicho tumboni mwake kitatolewa. Kuhusu namna anaishi maisha yake, mama huyo alisema hutegemea msaada wa majirani karimu ambao humupa chakula.Wajukuu wake pia humlinda. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments