WAPELEKANA POLISI BAADA YA JAMAA KULAMBA ASALI MASAA MAWILI MFULULIZO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 18, 2021

WAPELEKANA POLISI BAADA YA JAMAA KULAMBA ASALI MASAA MAWILI MFULULIZO

  Malunde       Friday, June 18, 2021


Mrembo aliyejulikana kwa jina la Joan Awuor ambaye hupakua asali kwa wanaume wenye kiu mtaani Dandora nchini Kenya amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufikishwa kituo cha polisi na mwanaume aitwaye Dennis Otieno ambaye ni mteja wake asiyeshiba utamu wa asali ya mabinti.

Inaelezwa kuwa Mrembo huyo Awuor alikutana na Otieno jijini na baada ya kumezea uzuri wake wakaamua kufanya biashara ya ngono. 

Mwanaume huyo alilipa KSh 4000 sawa na shilingi 86,000/= ya Tanzania na wakaelewana waende nyumbani kwa Awuor ili apakuliwe asali kukata kiu cha ngono.

Walipofika, hawakupoteza muda  wakaingia kazini mara moja huku binti huyo akifikiri Otieno ni kama wateja wake wa kawaida.

Kulingana na ripoti katika kituo cha polisi cha Dandora ambayo imenukuliwa na gazeti la People Daily, Otieno alilipa fedha za mzigo aliotaka kupitia Mpesa.

 Hata hivyo, baada ya masaa mawili kwenye kitanda, bado jamaa alikuwa akichemka vilivyo na huku binti akiishiwa na nguvu. 

"Afisa huyo hakumalizia kitendo kama kawaida licha ya kushiriki kwa masaa mawili. Awuor alimtoa na ndipo wakatofautiana," taarifa iliyo katika kituo cha polisi ilisema.

Otieno, ambaye ni afisa wa polisi jela katika kituo cha Lang'ata, alizusha akisema bado hajamaliza haja yake kwa mujibu wa malipo aliyokuwa ametoa.

 Ni hapo uzushi ulianza na wawili hao kufikishana katika kituo cha polisi huku Awuor akilalamika kuwa mteja wake alikuwa ameharibu vitu vyake vya nyumbani wakati wa kisanga hicho.

 Afisa mmoja katika kituo hicho alisema walikuwa na kesi ya kipekee kwani ni ngumu 'kushughulikia masuala ya kitandani kati ya mwanamke na mwanaume'.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post