MSANII KIVURANDE JUNIOR ALAZWA HOSPITALI

Mkali wa muziki wa kibaokata hapa nchini Kivurande Junior amehamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya hali yake kubadilika wakati alipokuwa amelazwa Hospitali ya Salamani iliyopo Magomeni jijini Dar es salaam.

Chanzo cha kulazwa kwa msanii Kivurande inaelezwa kuwa amepata tatizo la kushindwa kuvuta pumzi kwa sababu ya moshi uliomuingia wakati wa jaribio la kuzima moto ulioibuka katika nyumba aliyopanga kama frem ya biashara.

Via EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments