MFANYABIASHARA CHRIS KIRUBI AFARIKI DUNIA



Mfanyabiashara Chris Kirubi, enzi za uhai wake

Mfanyabiashara maarufu nchini Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Capital Group Limited, Chris Kirubi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 familia yake imethibitisha.

Mfanyabiashara huyo mnamo Novemba 2017 alisafirishwa kwenda Marekani kwa matibabu ya miezi minne akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.

Kwa kipindi hicho Kirubi alisema kwamba saratani aliyopata ilibainika mapema kiasi cha kuweza kutibika na kuweza kudhibitiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments