WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFUNGUA MILANGO MIPYA YA UWEKEZAJI KATIKA MAENEO YA UHIFADHI


Wizara ya Maliasili na Utalii imefungua milango mipya katika Sekta ya Utalii nchini kwa kutia saini ya  Uwekezaji wa kimkakati katika  maeneo ya Uhifadhi nchini kwa Wawekezaji wenye mitaji mikubwa wa kutoka ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro   wakati akitia saini  kanuni za Uwekezaji wa kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii amesema utiaji saini huo ni miongoni mwa  njia  zitakazochangia kuongeza idadi ya Watalii kufika milion 5  na mapato yapatayo bilion 6 ifikapo mwaka 2025 kupitia Sekta ya Utalii nchini.

Kwa mujibu wa Kanuni hizo Wawekezaji wataweza kuwekeza katika maeneo ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu pamoja na Maeneo ya Wazi ya Wanyamapori kwa miaka isiyopungua 25.

Akizungumza kabla ya utiaji saini huo, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema kanuni hizo zimelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa ambao hata watalii watakaokuja katika maeneo hayo ni Watalii wenye fedha nyingi ikiwemo watu maarufu duniani.

Amesisitiza kuwa kanuni hizo zitawezesha Wawekezaji hao kujenga mahoteli katika maeneo ya Uhifadhi pamoja na kuweka miundombinu ya Utalii itakayosaidia kuwavutia Watalii wengi kutembelea katika maeneo hayo.

Awali amesema kanuni hizo ni mpya na uwekezaji huo katika maeneo hayo utakuwa wa aina yake kwa vile umelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa watakaowavutia Watalii matajiri hali itakayopelekea pato la taifa kuongezeka maradufu kupitia sekta ya utalii nchini.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jenerali ( Mstaafu)  Hamis Semfuko amesema utiaji saini wa kanuni  ni moja ya hatua muhimu ya kupanua fursa zitokanazo na sekta ya utalii nchini.

” Tuliamua kuja na wazo hili ili Wawekezaji wenye mitaji mikubwa waweze kuwekeza katika maeneo ya Uhifadhi ambapo awali uwekezaji wa namna hii ulikuwa hauwezekani” alisisitiza Mwenyekiti huyo Meja Jenerali ( Mst) Semfuko

Kwa upande wake , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi amesema atahakikisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, ( TFS ) nao wanasaini kanuni za namna hiyo nao waweze kuwavutia Wawekezaji kuwekeza katika maeneo yao kwa vile wa maeneo yenye sifa kawa yalivyo ya TAWA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments