RC MAKALLA AMALIZA UGOMVI WA MEYA NA MKURUGENZI KINONDONI WALIOTUNISHIANA MISULI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, May 21, 2021

RC MAKALLA AMALIZA UGOMVI WA MEYA NA MKURUGENZI KINONDONI WALIOTUNISHIANA MISULI

  Malunde       Friday, May 21, 2021

Mvutano baina ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Sipora Liana na Meya wake Songoro Mnyonge, umemalizika baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kuingilia kati.


Liana na Mnyonge walitoleana maneno makali kwenye moja ya kikao cha Baraza la Madiwani kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za makusanyo mbalimbali.

Mapema leo Ijumaa, Makalla aliwaita kwenye kikao maalumu viongozi hao na kuzungumza kwa lengo la kumaliza mvutano huo, ambapo muafaka ulipatikana. Pia, aliwataka kwenda kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kinondoni waliyotumwa.

Kwa upande wa Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya Wananchi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post