MECHI YA SIMBA NA YANGA KUPIGWA LEO SAA MOJA USIKU


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.

TFF imesema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Tayari timu husika zimeshapewa taarifa ya mabadiliko hayo kupitia Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments