KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO AANZA KAZI, AONGOZA KIKAO CHA UTAMBULISHO KWA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA CCM | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, May 1, 2021

KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO AANZA KAZI, AONGOZA KIKAO CHA UTAMBULISHO KWA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA CCM

  Malunde       Saturday, May 1, 2021

 Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, jana jioni ameripoti ofisini na kuendesha kikao maalum cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.

Kikao hiko kimehudhuriwa na Wajumbe wapya akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), -Christina Mndeme na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Viongozi wastaafu wa CCM wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), – Rodrick Mpogolo na aliyekuwa Katibu wa NEC, Oganaizesheni Pereira Silima.

Chongolo amechaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Bashiru Ally.

Kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, Chongolo alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post