JAJI IMANI ABOUD APENDEKEZWA KUGOMBEA URAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA


Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania Mhe. Jaji Imani Aboud amependekezwa kugombea Urais wa Mahakama hiyo.


Jaji Aboud amesema endapo atashinda katika nafasi hiyo na kuibuka mshindi itakuwa ni heshma kubwa kwa nchi na kwake mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika kuhusu masula ya haki za binadamu…


Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema Tanzania inayo imani na Jaji Imani Aboud kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika masula ya kimahakama hivyo ushindi wake utakuwa ni sifa kwa Taifa na kwa wanawake kuendelea kushika nyadhifa kubwa sio Serikalini tu, bali kwenye taasisi na mashirika ya kimataifa.


Majaji wengine wanaogombea nafasi hiyo ni kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Malawi na Cameroon ambapo Hayati Jaji Augustino Ramadhani ndie alikuwa Mtanzania wa mwisho kushika nafasi hiyo ya Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments