ACHOMA MTOTO KISU KISHA KUJIUA ALIVYOBAINI AMEPATA MAAMBUKIZI YA VVU | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 4, 2021

ACHOMA MTOTO KISU KISHA KUJIUA ALIVYOBAINI AMEPATA MAAMBUKIZI YA VVU

  Malunde       Tuesday, May 4, 2021

Mwanaume aitwaye Shija Mwanzalima (30) mkazi wa Nyantorotoro mkoani Geita amejiua kwa kujinyonga baada ya kumjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea wiki iliyopita nyumbani kwa mama wa mtoto huyo Nyantorotoro.

"Chanzo cha tukio hili la kinyama ni msongo wa mawazo baada ya Shija Mwanzalima pamoja na mkewe kwenda hospitali kupima afya na kuonekana  maambukizi ya VVU huku mkewe akiwa mzima licha ya kuishi pamoja",amesema.

Amesema baada ya majibu walirudi nyumbani na kumtuma mkewe dukani kununua dawa na kisha yeye kufanya unyama huo ambapo mtoto alipata majeraha makubwa na amelazwa kwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post