SHILOLE ATHIBITISHA KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE ROMMY


Msanii Zuwena Mohamed 'Shilole' amethibitisha kufunga ndoa ya siri na mume wake Rajab Issa maarufu kama Rommy kama ambavyo ilikuwa inaelezwa na baadhi ya vyombo mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram muda mfupi uliopita Shilole ameandika hilo baada ya kufunga ndoa na mume wake.

"Alhamdulillah tumemaliza salama, rasmi ni mume na mke niliyechukuliwa kwa furaha na upendo wa juu 'Officially Husband and Wife happily taken and very much in love' kwasasa unaweza kuniita Mrs Rajab Issa (Rommy) Yarabbi iwe salama".

Kabla ya hapo Shilole alikuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara Uchebe na waliachana mwaka jana baada ya ugomvi mkubwa uliotokea kwenye ndoa.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post