RAIS SAMIA : TUMIENI AKILI NA MAARIFA KUKUSANYA KODI SIO NGUVU, MNAUA BIASHARA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao aliowateuwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma
**
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Wizara ya Fedha kuhakikisha inaongeza makusanyo hadi kufikia Sh.Trilioni mbili kwa mwezi lakini ukusanyaji huo utumie akili na maarifa badala ya nguvu na kusababisha biashara kufungwa.

Amesema nguvu kubwa ambazo zinatumika kukusanya mapato ya Serikali zimekuwa zikisababisha wafanyabiashara kufunga biashara zao na kwenda kuzifungua katika nchi nyingine,hivyo Serikali inakosa mapato.

Amesema hayo leo Aprili 1, 2021 Ikulu Chamwino Mjini Dodoma baada ya kuapishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga pamoja na mawaziri walioteuliwa jana ambao nao wameapa leo.

Rais Samia, amesema kwamba Makamu wa Rais wakati anazungumzia amesisitiza Serikali kuongeza ukusanyaji mapato kwa mwezi kufikia Sh.Trilioni mbili ambapo amesema hilo linawezekana lakini ametoa angalizo kwamba akili na maarifa ndio inatakiwa kutumika kuongeza ukusanyaji huo wa mapato ya Serikali.

Amemsisitiza Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba lazima wasimamie ukusanyaji mapato vizuri, hakuna sababu ya kutumia nguvu katika kukusanya kodi."Nguvu kubwa sana inatumika na badala ya kusaidia wafanyabiashara mnasababisha wafunge biashara zao na sio kufunga tu biashara za watu kwasababu sheria inaruhusu,hapana .tumieni weledi na maarifa katika ukusanyaji wa kodi."

Akimzumngumzia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, Rais Samia amesema amemsikiliza wakati anazungumza na bahati nzuri amezungumzia kutokuwepo kwa mfumo wa ufanyaji kazi serikalini na huo ndio ugonjwa mkubwa."Katibu Mkuu Kiongozi najua wewe ndio daktari ambaye unakwenda kutibu huu ugonjwa, lazima Serikali ifanye kazi kwa pamoja."

Wakati huo amesema kwamba katika mazungumzo yake amekuwa akitaja Bunge la Katiba huenda ni kwasababu amepushiwa( msukumo) lakini ameweka wazi hilo la Katiba Mpya kwa sasa wasahau kwanza.

 Chanzo - Michuzi Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments