MARAIS 11 KUAGA MWILI WA MAGUFULI KESHO DODOMA


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Kulia ni Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi
***
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema hadi sasa marais 11 wemethibitisha kuungana na Watanzania katika kumuaga na kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Dk. Abbas amesema msiba huu si wa Watanzania pekee yake bali umeigusa dunia nzima ambapo kwa upande wa Jumuiya za Afrika, balozi na asasi za kikanda watakuwa zaidi ya 50 ambao wamethibitisha ushiriki wao.

"Msiba huu si wa Tanzania tu msiba huu umeigusa dunia nzima, kesho tunatarajia viongozi mbalimbali wa kimataifa watashirikiana nasi Watanzania kumuaga, kumuombeleza kiongozi wetu, ningependa kuwataja baadhi ya viongozi ambao hadi mchana huu wamethibitisha kwamba wataungana nasi hapa Dodoma, tutakuwa na marais na viongozi wanaowakilisha marais wao watakuwa 11," amesema Dkt. Abbas.

Amesema kwa upande wa marais watakao kuja ni pamoja na Mhe.Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya, Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, Rais wa Comoro Azali Assoumani, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na Rais wa Zambia Edgar Lungu.

Wengine ni Rais wa Namibia Hage Geingob, Rais Botswana Mokwaeetsi Masisi, Rais Afrika Cyril Ramaphosa Kusini, Rais wa DRC Felix Tshisekedi na viongozi watakaowakilisha Marais Waziri Mkuu wa Rwanda, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola na Makamu wa Rais wa Burundi.

Aidha, amewakaribisha wananchi kukaa barabrani ili kumpungia na kumuaga kiongozi wao mara mwili utapowasili Jijini Dodoma leo na kesho asubuhi mara watapokuwa wanaelekea bungeni na kwenye uwanja wa Jamhuri huku akiwasisitiza kuendelee kumuombea dua Hayati Dkt. Magufuli.

UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post