RAIS KAGAME NA MKE WAKE WAPATA CHANJO YA CORONA


Rais Paul Kagame akichanjwa chanjo dhidi ya corona

Mke wa rais wa Rwanda, Janeth Kagame

Rais  wa Rwanda Paul Kagame amechanjwa chanjo dhidi ya Corona ikiwa sehemu ya mpango wa uchanjaji wa taifa zima la Rwanda ambapo zaidi ya watu 230,000 wamepatiwa chanjo hiyo ya kujikinga na Corona.

Rais Kagame na mkewe Jannette Kagame wamepatiwa chanjo ya COVID-19 katika Hospitali ya Mfalme Faisal.

Rwanda inatarajia kupata dozi za chanjo ya corona 1,098,960, aina ya AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech, zitatolewa kwa awamu wa kwanza na wa pili wa mwaka 2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post