Picha : DC ANAMRINGI MACHA AZINDUA MRADI WA MAJI VIJIJI VYA IRAMBA NA IGWAMANONI - USHETU


Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizindua mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu
****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amezindua mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa gharama ya shilingi milioni 365.7 ukitarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya 5,214.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amezindua mradi huo wa maji safi na salama ambao chanzo chake ni kisima kirefu leo Jumatano Machi 17,2021 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji nchini ambayo kilele chake ni Machi 22 ambayo ni Siku ya Maji Duniani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Macha amesema mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto ya muda mrefu ya wananchi kutumia muda mwingi kutafuta maji na sasa wananchi watatumia maji hayo kwa mambo ya kijamii na kiuchumi.

“Tumetekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo iliahidi kuwaletea maji wananchi.Wito wangu kwenu ni kutunza miundo mbinu ya maji hivyo kila mtu awe mlinzi wa mwenzake ili mradi huu udumu kwa muda mrefu. Kazi ya serikali ni kuendelea kusambaza maji katika maeneo mengine”,amesema Macha.

“Kamati ya maji aambayo itafanya kazi ya kusimamia mradi ikishirikiana na Wataalamu kutoka RUWASA naomba muwe waaminifu,simamieni vizuri fedha za mradi”,ameongeza.

Mkuu huyo wa wilaya aliwasisitiza wananchi kuvuta maji hadi majumbani mwao huku akiweka wazi kuwa ndoo moja ya maji itauzwa kwa kiasi cha shilingi 50.

Katika hatua nyingine Macha amesema kazi kubwa ya Serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuboresha huduma za maji, elimu, umeme,elimu na miundo mbinu ya barabara hivyo kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na serikali ili kufikia haraka maendeleo yaliyokusudiwa.

Akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Maji katika Vijiji vya Iramba na Igwamanoni, Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Aprili 1, 2020 na umetekelezwa naa Wataalamu wa ndani wa RUWASA kwa mfumo wa Force Account kwa ufadhili wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mpango wa Malipo kwa Matokeo.

Amesema mradi huo unahusisha uchimbaji wa mtaro,ulazaji wa bomba kuu la kupandisha maji kwenye tenki la maji na ulazaji bomba kwenye mtandao wa kusambaza maji pamoja na kufukia mtaro,ujenzi wa tenki la maji,ujenzi wa vyumba vya mitambo,ujenzi wa vituo vya kuchotea maji,ujenzi wa ofisi ya Jumuiya ya Watumiaji Maji,kununua na kufunga pampu ya kusukuma maji na kuunganisha umme wa gridi ya taifa kwenye chanzo cha maji.

“Mpaka sasa fedha zilizotumika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi ni shilingi 365,778,635.02. Ujenzi wa mradi huu umekamilika kwa asilimia 98 na unaendelea kutoa huduma za maji kwa wananchi. Kazi inayoendelea ni ujenzi wa chemba kwenye mtandao wa usambazaji maji pamoja na utengenezaji wa vigingi kwa ajili ya alama za kuonesha bomba zinamopita”,ameeleza Mhandisi  Magili.

Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mkurya ameishukuru serikali na wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kupata katika utekelezaji wa miradi ya maji na kuwataka wananchi kutunza miundo mbinu ya maji na kutunza mazingira kwa kupanda miti.

Naye Diwani wa Kata ya Igwamanoni ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Gagi Lala pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama, Thomas Myonga wamesema kupatikana kwa maji sasa kunaondoa kero ya maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni ambapo wananchi walikuwa wanatumia muda mwingi kutafuta maji na wakati mwingine kusababisha migogoro ya ndoa, wanaume wakiwatuhumu wake zao kuchepuka kwa kisingizio cha maji.

Nao wakazi wa Igwamanoni akiwemo Benadetha Paul wamesema sasa wana raha maji yamepatikana kwani awali walikuwa wanakutana hadi na wanyama wakali wakiwemo fisi na baadhi ya wanawake kufanyiwa ukatili wakati wakitafuta maji.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizindua mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu leo Jumatano Machi 17,2021 uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa gharama ya shilingi milioni 365.7. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza katika kituo cha kuchotea maji cha Senta ya Iramba wakati akizindua mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akifungua bomba la maji wakati akizindua mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu leo Jumatano Machi 17,2021 uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa gharama ya shilingi milioni 365.7.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama (aliyevaa nguo ya kijani) wakifungua maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu leo Jumatano Machi 17,2021 uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa gharama ya shilingi milioni 365.7.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimtwisha kichwani ndoo ya maji mmoja wa wananchi wakati akizindua mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (wa pili kushoto) akizungumza baada ya kuzindua mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu leo Jumatano Machi 17,2021 uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa gharama ya shilingi milioni 365.7.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu
Wananchi wakichota maji katika kituo cha kuchotea maji cha Senta ya Iramba kata ya Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Muonekano katika sehemu ya kituo cha kuchotea maji cha Senta ya Iramba kata ya Igwamanoni.
Muonekano katika sehemu ya kituo cha kuchotea maji cha Senta ya Iramba kata ya Igwamanoni.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe . Anamringi Macha kuhusu ujenzi wa mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni unaotekelezwa na RUWASA.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili (kulia) akimuonesha Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe . Anamringi Macha kisima kirefu cha mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni unaotekelezwa na RUWASA.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili (kulia) akimuonesha Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe . Anamringi Macha kisima kirefu cha mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni unaotekelezwa na RUWASA.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe . Anamringi Macha akipanda mti katika Chanzo cha Maji cha Mradi wa Maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni katika halmashauri ya Ushetu
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili (kulia) akimweleza jambo Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe . Anamringi Macha wakati Mkuu huyo wa wilaya akitoka kukagua ujenzi wa Tenki la Maji
Muonekano wa Tenki la maji la mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni unaotekelezwa na RUWASA.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili (kulia) akielezea kuhusu ujenzi wa nyumba ya Jumuiya ya Watumiaji wa Maji
Muonekano wa nyumba ya Jumuiya ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni unaotekelezwa na RUWASA.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe . Anamringi Macha akizungumza baada ya kutembelea nyumba ya jumuiya ya watumiaji maji katika mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni unaotekelezwa na RUWASA.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe . Anamringi Macha akizungumza na wananchi wa Senta ya Iramba baada ya kuzindua mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mkazi wa Iramba, Benadetha Paul akiishukuru serikali kutekeleza mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni ambao sasa unaondoa changamoto ya maji ya muda mrefu iliyokuwa inawakabili.
Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mkurya akiishukuru serikali na wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kupata katika utekelezaji wa miradi ya maji.
Diwani wa Kata ya Igwamanoni ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Gagi Lala akiishukuru serikali kutekeleza mradi wa maji wa vijiji vya Iramba na Igwamanoni.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama, Thomas Myonga akiishukuru serikali kutekeleza Ilani ya CCM kwa kupeleka maji katika vijiji vya Iramba na Igwamanoni.
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Viongozi na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Viongozi na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde  1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post