MAMA WA MIAKA 50 NA WATOTO WATANO ARUDI SHULE KUSOMA SHULE YA MSINGI

Mwanamke aitwaye Justina Onwumere, (50) nchini Nigeria anagonga vichwa vya habari mtandaoni baada ya kurejea shuleni akiwa na miaka 50 ambapo alishindwa kuendela na masomo yake ya msingi wakati akiwa mchanga kwa sababu ya kuolewa mapema.

Mwanae wa kiume kwa jina Chima Onwumere, ndiye alitangaza taarifa hiyo kupitia Facebook, huku akimsherehekea mama yake.

Chima alisimulia namna mama yake alimpigia simu mwaka 2020 kumfahamisha kuhusu hamu yake ya kutaka kurejea shuleni. 

Huo ulikuwa wakati wa furaha kwake Chima huku mama yake akiamua kufuata ndoto yake aliyokuwa amewacha miaka mingi iliyopita. 

Alifurahia kwamba hii itakuwa rekodi ya Justina huku mama huyo wa watano akisema ni mtu ambaye anapenda sana masomo.

 "Mwaka jana nilipata simu kutoka kwa mama yangu akisema kuwa anataka kurejea shuleni kwa sababu alipoteza nafasi hiyo kutokana na ndoa ya mapema.

"Nilifurahia sana kama mpenzi wa masomo na umuhimu wake, nilimwamba nitaunga mkono uamuzi wake," aliandika mwanawe Justina. 

Chanzo- Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post