WALIOKAMATWA WAKISAFIRISHA NYOKA NA VINYONGA KUFIKISHWA MAHAKAMANI



Wizara ya Maliasili na Utalii imewakamata Watanzania wanne wanaotuhumiwa kusafirisha vinyonga hai 74 na nyoka sita kinyume cha sheria na kuwauzia raia wawili wa Czech.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa, vinyonga na nyoka hao walikamatwa Januari 22 mwaka huu nchini Austria na kuhifadhiwa katika hifadhi ndogo ya wanyama nchini humo.

Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho, wakikabiliwa na makosa ya kusafirisha nje wanyamapori hao bila kibali, uhujumu uchumi pamoja na utakatishaji fedha kupitia biashara hiyo.

Dkt. Ndumbaro ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayebainika kufanya biashara ya kusafirisha Wanyamapori hai ndani na nje ya nchi, wakati biashara hiyo imezuiliwa tangu Mei 2016 atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments