MZEE MWINYI : KIPINDI CHA UONGOZI WA MAGUFULI NCHI IMEPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO NA KUUSHANGAZA ULIMWENGU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, March 27, 2021

MZEE MWINYI : KIPINDI CHA UONGOZI WA MAGUFULI NCHI IMEPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO NA KUUSHANGAZA ULIMWENGU

  Malunde       Saturday, March 27, 2021
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ally Hassan Mwinyi amesema katika kipindi cha uongozi wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli, nchi imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kuushangaza ulimwengu.

Akitoa salamu jana March 27, 2021 katika uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita ilipofanyika Misa Takatifu ya Mazishi ya Dkt Magufuli, Mzee Mwinyi alisema kiongozi huyo alikuwa si mtu wa maneno, bali alikuwa  mtu wa vitendo na aliyependa matokeo.

Mzee Mwinyi alisema katika kipindi kifupi cha takribani miaka mitano Dkt Magufuli ameweza kufanya mambo makubwa ambayo watangulizi wake walishindwa kuyafanya kwa takribani miaka 40 , ikiwa ni pamoja na kutekeleza kwa vitendo ndoto ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuhamishia Makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma.

Mambo mengine ni kuiunganisha Tanzania kwa barabara za lami na kuboresha usafiri wa anga kwa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Rais Mstaafu Mwinyi alisema kifo cha Dkt Magufuli binafsi kimemsikitisha sana, kwani alikuwa ni kiongozi aliyempenda sana.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post