KELVIN CHALE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI UVCCM WILAYA YA SONGEA MJINI


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya   Songea Mjini Kelvin Chale akizungumza baada ya kumalizika uchaguzi
Joseph Chale (kushoto) akimpongeza kaka yake Kelvin Chale baada ya kutangazwa mshindi nafasi ya Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Songea mjini 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya  ya Songea Mjini Kelvin Chale.
***
Na Mwandishi wetu Songea 
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kelvin Chale amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya   Songea Mjini baada ya kuwabwaga wenzake watatu akipata kura 185.
 
Uchaguzi huo umefanyika leo ukumbi wa Open University Manispaa ya Songea kwa lengo la kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Issa Chiwaneke kushinda kiti cha Udiwani kata ya Ndilima Litembo.


Akitangaza Matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi ,Mwanahamisi Manyopo  alimtangaza Mshindi kuwa ni Kelvin Chale aliyepata kura 185, Kalela Khalifa kura 130, akifuatiwa Renatus Chale aliyepata  kura 32 na Rustika Komba kura 1.

 Alisema wajumbe waliopiga kura ni 354 kura zilizoharibika 6 kura halali 348.

Kwa upande wake Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti Kelvin Chale amewaomba wagombea wenzake kushirikiana naye katika kukijenga chama akibainisha kuwa atahakikisha anawapigania vijana kupata mkopo asilimia 4 kutoka mwenye halmashauri iliziwasaidie kuanzisha Biashara ndogo ndogo.

Aidha amesem atatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa kushirikiana na viongozi wenzake ili mikopo watakayopata iwe na manufaa kuinua uchumi wa vijana wenzie,ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha pamoja kwani Jumuia hiyo kwa sasa imegawanyika, yeye atawaunganisha pamoja na kuwaletea maendeleo.

Soma pia:Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post