WABUNGE 19 WALIOVULIWA UANACHAMA CHADEMA WAINGIA BUNGENI


Wabunge 19 wa Viti Maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), asubuhi ya leo wamefika na kuendelea na kikao cha Bunge kilichoanza leo Jumanne, Februari 2, 2021 Jijini Dodoma.

Wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee wameingia mjengoni wakiwa wamevalia mavazi meusi huku Mdee akiwa amevaa barakoa .

Itakumbukwa Wabunge hao tayari walishavuliwa uanachama na chama chao mwishoni mwa mwaka jana kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama chao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post