BABU AFARIKI AKIFANYA MAPENZI KWENYE GESTI ANAYOILINDA

 


Maafisa wa polisi katika kaunti ya Nyandarua nchini Kenya wanachunguza hali iliyopelekea kifo cha mzee mmoja mwenye miaka 58, ambaye ameaga dunia akifanya mapenzi.

 Kulingana na ripoti ya polisi, Edith Wairimu Mwangi (55) alimpata marehemu akihema sana baada ya kwenda kusafisha chumba hicho katika nyumba ya kulala wageni ya Heshima Lodge Olkalau. 

Kufuatia hali hiyo mwanamke huyo alikimbia katika Kituo cha Polisi cha Olkalau kutoa  ripoti ambapo maafisa wa polisi walikimbia katika eneo la tukio wakiandamana pamoja na makachero kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI). 

Ambulensi ilitafutwa na alikimbizwa katika Hospitali ya JM Kariuki ambapo alithibitishwa kufariki dunia. 

"Wakati mwili wake ulikuwa unakaguliwa, alipatikana na kondomu kwenye uume wake. Eneo la tukio lilichunguzwa na maafisa wa CSI kabla ya mwili huo kupelekwa mochari ukisubiri kufanyiwa upasuaji," ilisoma ripoti ya polisi. 

Mwanamume huyo pia alikuwa mlinzi wa Lodge hiyo na bado haijajulikana alikuwa na mwanamke yupi. 

Kisa hiki kinakuja siku chache baada ya mwanamume mwingine mwenye miaka 52, kuzirai na kufariki usiku wa Jumatano, Februari 3. 

Ernest Kamanda anasemekana alianza kukumbwa na matatizo ya kiafya majira ya saa 11:30 jioni Jumatano wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo. 

Kulingana na ripoti ya polisi ambayo TUKO.co.ke iliiona, mwanamke huyo aliyetambulika kama Catherine Kinyanjui mwenye umri wa miaka 47, alikimbizwa katika hospitali ya Shalom akisaidiwa na majirani ambapo alisemakana alikata roho. 

Wiki mbili zilizopita tuliripoti kisa kingine ambapo mzee mwenye umri wa miaka 80 aliaga dunia katika njia isiyoeleweka akijivinjari na mrembo wa miaka 33 katika hoteli moja Dar es Salaam, Tanzania. 

David Mluli alipatikana ameaga dunia Jumamosi, Januari 16 katika chumba nambari 22 Mbezi Garden ambapo alikuwa ameenda kufurahia na mrembo kwa jina Neema Kibaya ambaye alikamatwa kutokana na kisa hicho.
Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post