Picha : WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA RAFIKI SDO WAKUTANA SHINYANGA KUSHEREHEKEA 'RAFIKI SDO FAMILY DAY'



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a akifungua kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day'

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Rafiki SDO limeadhimisha siku ya Familia ya wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day 2021' kwa kukutana na wafanyakazi wake wanaotekeleza miradi katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Rukwa na mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufahamiana na kuelezana mafanikio na changamoto walizopitia katika mwaka uliopita.

Rafiki SDO Family Day imeanza kwa kikao ambacho kimefanyika leo Jumamosi Februari 6,2021 katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a.

Akifungua kikao kazi hicho, Ng’ong’a alisema shirika la Rafiki SDO limekuwa na utaratibu wa kukutana na wafanyakazi wake kila mwaka kwa lengo la  kufanya kikao cha pamoja na kuwasilisha taarifa mbalimbali, kuwapa zawadi kwa wafanyakazi bora na kufanya sherehe ya wafanyakazi kupongezana maarufu ‘Rafiki Family Day’.

“Katika kikao hiki tunafanya uwasilishaji wa shughuli zinazofanywa na Rafiki SDO,kuchagua Rafiki wa Mwaka 2021 lakini pia kufanya sherehe ya familia ya Rafiki SDO na kutoa zawadi kwa Rafiki wa mwaka”,alieleza Ng’ong’a.

Aidha alisema shirika la Rafiki SDO linaendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa miaka mitano ‘Strategic Plan 2020/2024’ unaojikita katika maeneo nane muhimu ikiwemo sekta ya afya,elimu,maji na usafi wa mazingira,masuala ya jinsia,VVU na UKIMWI,watoto wanaoishi katika mazingira magumu na uimarishaji wa shirika hilo.

Ng’ong’a alisema utendaji kazi bora wa wafanyakazi wa Rafiki SDO ndiyo umesababisha shirika hilo liendelee kusifika kwa kazi nzuri ndiyo maana mbali na ofisi ya Shinyanga Mjini pia wamefungua ofisi katika mikoa mingine ikiwemo mkoa wa  Mara (Musoma), Rukwa na wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Aliwataka wafanyakazi kutekeleza majukumu yaliyowaleta katika shirika hilo na kuepuka kujiingiza katika vitendo vyovyote vya ukatili ndani na nje ya shirika sambamba na kuepuka vitendo vya udanganyifu wa aina yoyote huku akiwasisitza kufanya kazi kwa utii na heshima kwa kuzingatia sera za shirika na sheria za nchi.

 Naye Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Rafiki SDO , Happiness Misael ameuongeza uongozi wa shirika hilo namna linavyoongoza wafanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kusimamia kikamilifu stahiki za watumishi wake.

Kwa upande wao wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wamesema kupitia kikao hicho wameweza kuifahamu Rafiki SDO na miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika pamoja na kufahamiana. 

Shirika la Rafiki SDO linatekeleza miradi mbalimbali mkoani Mara ,Rukwa na Shinyanga ukiwemo mradi wa Kuzuia na kupinga mimba na ndoa za utotoni ,Acha Wasome, Kupinga ajira za watoto migodini, Dreams na Tuwalee.

Mradi mwingine ni COVID-19 na EpiC unaojihusisha na masuala ya ukatili wa kijinsia, shughuli za kitabibu ikiwemo kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, kuyafikia makundi maalumu kama wanawake wanaofanya biashara ya ngono na kuwapa elimu ya mabadiliko ya tabia na kuwawezesha kiuchumi. 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a akifungua kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya  Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day' kilichofanyika katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Februari 6,2021. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a akifungua kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya  Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day' kilichofanyika katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Februari 6,2021. Kushoto ni Meneja Miradi Msaidizi wa Shirika la Rafiki SDO George Nyamboto, kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO Ahsante Nselu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a akifungua kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya  Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day' kilichofanyika katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Februari 6,2021. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a akifungua kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya  Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day' kilichofanyika katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Februari 6,2021. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a akimtambulisha Meneja Miradi Msaidizi wa Shirika la Rafiki SDO George Nyamboto (kushoto) na Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO Ahsante Nselu (kulia).
Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO Ahsante Nselu akizungumza katika kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya  Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day' kilichofanyika katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Februari 6,2021.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya Rafiki SDO Family Day Tangi Clement akizungumza kwenye kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya  Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day' kilichofanyika katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Februari 6,2021.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya Rafiki SDO Family Day Tangi Clement (kushoto) akitambulisha wajumbe wa kamati hiyo kwenye kikao kazi cha wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya  Wafanyakazi wa Shirika hilo 'Rafiki SDO Family Day' kilichofanyika katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Februari 6,2021.
 Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Rafiki SDO, Happiness Misael akizungumza katika kikao hicho ambapo ameuongeza uongozi wa shirika hilo namna linavyoongoza wafanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kusimamia kikamilifu stahiki za watumishi wake.
Afisa Tawala na Fedha wa Shirika la Rafiki SDO Lydia Pius akizungumza katika kikao hicho.
Wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wakiwa ukumbini.
Mwafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO wakiwa ukumbini
Joseph Madaga akiwasilisha taarifa kuhusu Mradi wa Acha Wasome unaotekelezwa katika Manispaa ya Musoma  lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanamaliza shule  kuanzia kidato cha kwanza hadi nne katika shule 15 ambapo wanafunzi wanajengewa uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababisha wasimalize shule. 
Mratibu wa Mradi Kuzuia na Kupinga Mimba na Ndoa za Utotoni Shirika la Rafiki SDO Mkoa wa Rukwa Nyamagari  Chombo akielezea kuhusu mradi wa kuzuia na kupinga ndoa za utotoni.

Picha zifuatazo hapa chini ni Maafisa wa Shirika la Rafiki SDO wakiwasilisha taarifa za miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo mkoani Shinyanga, Rukwa na Mara
Mtoa huduma za afya Shirika la Rafiki SDO, Joyce Ernest akizungumza ukumbini
Wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO wakicheza muziki ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments