WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI DK. CHAMURIHO AWATAKA WAFANYAKAZI SEKTA YA UCHUKUZI KUJIENDELEZA KIELIMU


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  Dk. Leonard Chamuriho akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi katika ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Mwanza  Januari11, 2021.
Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi  Gabriel Migire akizungumza kwenye Mkutano huo
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini.


Na Hellen Mtereko Mwanza

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ,Dkt. Leonard Chamuriho amewataka  wafanyakazi wa sekta ya Uchukuzi kujenga tabia ya kujiendeleza kielimu ili  wafanye kazi kwa weledi.

Ameyasema hayo leo  Januari 11,2021 wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa sekta hiyo Jijini Mwanza  wenye lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu ya kazi, utawala na wajibu wa wafanyakazi.

Alisema kila mtumishi ana wajibu wa kufanya kazi kwa weledi na  ushirikiano ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya sekta hiyo.
 
Alisema hatutasita kuchukua hatua pale tutakapobaini mazoea yanawekwa mbele badala ya weledi katika utendaji wa kazi.

Aliongeza kuwa ni lazima wajibu uambatane na uelewa wa majukumu ya kila mmoja  pamoja na uhusiano mwema kazini Kati ya viongozi na wafanyakazi.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa sekta hiyo Gabriel Migire alisema  katika mpango wa tatu wa maendeleo ya Taifa unaoendelea kuandaliwa sekita hiyo imepewa dhamana ya kutekeleza miradi ya kielelezo ikiwemo ujenzi wa reli ya Kati, uboreshwaji wa Bandari ya Dar -es Salaam na uimarishaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo unasimamiwa na wajumbe  wa sekta hiyo hivyo amewaasa  kutekeleza miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa na kulinda thamani ya fedha iliyowekezwa.

Naye Mjumbe kutoka Sekta ya Uchukuzi Stella Katondo alisema  atahakikisha wanafanya kazi kwa weledi na bidii ili waweze kukamilisha miradi iliyopo kwenye sekta hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments