WALIMU WAWILI MKOANI NJOMBE WATIWA MBARONI KWA KUMTOA MIMBA MWANAFUNZI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, January 22, 2021

WALIMU WAWILI MKOANI NJOMBE WATIWA MBARONI KWA KUMTOA MIMBA MWANAFUNZI

  Malunde       Friday, January 22, 2021


Na Amiri Kilagalila, Njombe
JESHI la Polisi mkoani Njombe linawashikilia walimu wawili wa shule ya sekondari Mang’oto wilayani Makete mkoani Njombe kwa tuhuma za kumsababishia ujauzito na kumtoa mwanafunzi wa shule hiyo mwenye umri wa miaka 17.

Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe,  Hamis Issa amesema wanamshikilia mwalimu Ezekiel Thomas (36) maarufu kwa jina la Dokole kwa kuwa na mahusiano na mwananfunzi na kumsababishia ujauzito.

“Huyu mwalimu amekuwa na mahusiano na mtoto wa sekondari mwenye umri wa miaka 17 na binti huyo amepimwa amegundulika ni mjamzito.” Alisema kamanda Issa

Aidha amesema wanamshikilia mwalimu, Ben Liamdilo (35) kwa kushirikiana katika tukio la utoaji wa mimba na kumsababishia maumivu mwanafunzi huyo.

“Mwalimu Thomas alifanya juhudi akamtuma huyu mwalimu mwenzake akambeba na boda boda kwenda kumtoa mimba mpaka sasa hivi walimu wote wawili tunawashikilia na wanatuhumiwa na makosa haya.”Alisema kamanda Issa

Vile vile ameitaka jamii kushirikiana kwa kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi ili kukabiliana na vitendo kama hivyo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post