MSHAHARA WA CHIKWENDE SIMBA SC BALAA MTUPU


UNAWEZA kusema ni kufuru mara baada ya uongozi wa Simba kukubali kumpa staa mpya wa timu hiyo, Perfect Chikwende mshahara wa dola za Kimarekani 8,000 ambazo ni sawa na Sh 18,470,900 za Kitanzania.

Chanzo cha kumaminika kutoka ndani ya Simba, kilieleza kuwa ulitokea mvutano mkubwa kwenye mshahara huo ambao Simba walitaka kumpa dola 6,000 (Sh 13,853,200), lakini jamaa akaweka ngumu akitaka dola 8,000 huku akiwaambia kama wakishindwa atakwenda zake Azam ambao walikuwa tayari kutoa mpunga huo.

Kikizungumza na Spoti Xtra, chanzo hicho kilisema mshahara wa Chikwende ni mkubwa zaidi pengine kuliko wachezaji wengine.

“Chikwende atakuwa analipwa dola za Marekani 8,000, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 18 za Kitanzania, Simba walikuwa wanataka wampe chini ya hapo, kwenye dola 6,000 au 5,000, lakini jamaa akagoma kabisa akidai kama wakishindwa kumpa anachotaka atakwenda zake Azam,” kilisema chanzo hicho.

Simba imesajili Chikwende kwa mkataba wa miaka miwili unaotajwa kufikia thamani ya dola 55,000 ambazo ni sawa na Sh 126,987,000 na inaelezwa kama Simba wangezubaa kidogo mwamba huyo alikuwa anatua ndani ya Azam FC.


STORI: MUSA MATEJA NA ISSA LIPONDA
CHANZO - Global Publishers

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post