MAZUNGUMZO YA TRUMP YA SIRI GEORGIA, KUJARIBU KUBADILISHA MATOKEO YA UCHAGUZI YANASWA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, January 4, 2021

MAZUNGUMZO YA TRUMP YA SIRI GEORGIA, KUJARIBU KUBADILISHA MATOKEO YA UCHAGUZI YANASWA

  Malunde       Monday, January 4, 2021


Kanda ya sauti imepatikana ambamo Rais Donald Trump wa Marekani anasikika akimshinikiza kamishna wa uchaguzi katika jimbo la Georgia kutafuta kura za kumsaidia Trump kushinda jimbo hilo katika uchaguzi wa rais wa Novemba iliyopita.

 Katika kanda hiyo Trump anasikika katika mazungumzo ya simu na kamishna huyo, Brad Raffensperger akimtaka waziwazi kutafuta kura karibu 12,000 na kurudia mahesabu ya kura ili Trump atangazwe mshindi. 

Kanda hiyo imewekwa hadharani na gazeti la Washington Post kuthibitisha hatua hiyo ya Rais Donald Trump, ambaye amepoteza kwa kura chache jimbo hilo la kusini mashariki mwa Marekani ambalo miaka ya nyuma lilikuwa ngome ya kutegemewa ya chama cha Republican chake rais Trump. 

Makamu wa rais mteule, Kamala Harris amesema kitendo hicho cha Rais Trump ni matumizi mabaya ya madaraka.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post