MWILI WA MSANII C PWAA WAZIKWA MAKABURI YA MWINYI MKUU MAGOMENI DAR ES SALAAM


Mazishi ya Msanii wa Bongo Fleva, Ilunga Khalifa maarufu C Pwaa yamefanyika jioni ya leo kwenye makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni, Dar es salaam. Cpwaa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Januari 17, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kaka mdogo wa msanii huyo ambaye alikuwa akimuuguza kipindi chote cha maradhi, Murad Omar Khamis amesema kaka yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (pnemounia) kwa wiki sasa lakini alizidiwa wiki hii na walimkimbiza hospitali ambapo alilazwa kabla ya umauti kumfika usiku wa kuamkia leo Januari 17.

"Alikuwa anaumwa wiki mbili zilizopita, na akaja kuishi hapa nyumbani kwa mama yake. Ila Jumatano alizidiwa ndiyo tukamkimbiza hospitali muhimbili, alilazwa ICU," aliongeza.
Msanii Cpwaa enzi za uhai wake
TAZAMA VIDEO HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments