JESHI LA ZIMAMOTO LAFANYA MKUTANO MKUU ZIMAMOTO SACCOS LTD... LAHAMASISHA ASKARI KUJIUNGA NA SACCOS YAO


Mwenyekiti wa bodi  Zimamoto Sacco's Christina Sunga akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka Zimamoto SACCOS LTD 2021leo Jijini Mwanza kwa lengo la kuhamasisha Watumishi wa Jeshi hilo kujiunga na kununua hisa za  Zimamoto Saccos limited.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wili wa Mwaka Zimamoto SACCOS LTD 2021 leo January Januari 9,2021 Jijini  Mwanza kwa lengo la kuhamasisha Watumishi wa Jeshi hilo kujiunga na kununua hisa za  Zimamoto Saccos limited.
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini.
Bilhah Chailla kutoka Mtwara akipokea cheti 


Na Hellen Mtereko Mwanza

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania  limefanya Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka Zimamoto SACCOS LTD 2021 leo Jumamosi Januari 9,2021 Jijini  Mwanza kwa lengo la kuhamasisha Watumishi wa Jeshi hilo kujiunga na kununua hisa za  Zimamoto Saccos limited.

Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo John Masunga ambae alikuwa mgeni  rasmi  kwenye mkutano huo amehamasisha  watumishi wa Jeshi hilo kujiunga na mfuko huo ili uweze kuwahudumia na kukidhi mahitaji yao.

Alisema kwamba Saccos hiyo ambayo ilianza mwaka 2019 bado ni changa lakini imeanza vizuri kwani imepata muitikio wa kutosha kutoka kwa Wanachama waliokwisha jiunga na mfuko huo.

Masunga Alisema kuwa uwepo wa Saccos hiyo itawasaidia Watumishi hao  kupata mikopo kwa riba nafuu ukilinganisha na Taasisi nyingine za kifedha.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa bodi ya Saccos hiyo Christina Sunga alisema kuwa Saccos hiyo ilianzishwa kwa malengo ya kuweza kusaidia kukuza uchumi katika jamii ya jeshi hilo.

 Aidha, Alisema kuwa Saccos hiyo Ina mtaji wa million 35.4 na fedha hizo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili askari  ili waweze kuondokana na kero zinazohusisha ukopaji wa fedha wenye riba kubwa kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha.

Sunga aliongeza kuwa Saccos hiyo kwa Sasa inawanachma 207 huku waliolipia hisa wakiwa 124 na 83 bado hawajalipia hisa zao.

Sunga amebainisha kuwa huduma zitolewazo ni upokeaji na utunzaji wa hisa,akiba utoaji wa mikopo ya hisa mbalimbali.

Alitaja aina ya mikopo inayotolewa na Saccos hiyo kuwa ni mikopo ya Elimu, mkopo wa dharula na mikopo maalum ambayo yote riba  yake ni asilimia mbili.

Mwanachama wa zimamoto Saccos limited Insipekita Hamis Dawa kutoka Kagera ametoa rai kwa wanachama wenzake kumalizia michango yao ya kulipia hisa ili waweze kunufaika na mikopo kutoka kwenye mfuko huo.

Bilhah Chailla ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi hilo kutoka Mtwara ametunukiwa cheti  baada ya kukidhi vigezo vya kununua hisa 10 ambazo ni sehemu ya umiliki wa mtaji wa chama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments