UCHAGUZI UGANDA : SERIKALI YAAGIZA MITANDAO YOTE YA KIJAMII KUFUNGWA


Uganda imeagiza watoaji huduma za mtandao kufunga mitandao yote ya kijamii na programu za kutuma ujumbe kufikia Jumanne hadi wakati usiojulikana, kwa mujibu wa barua kutoka kwa mdhibiti wa mawasiliano nchini humo iliyonukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Watumiaji walikuwa wamelalamika awali Jumanne, kwamba hawaweza kupata mtandao wa Facebook na WhatsApp, majukwaa ya mitandao ya kijamii inayotumiwa sana katika kipindi cha kampeni kabla ya uchaguzi wa urais kwenye nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

"Tume ya mawasiliano Uganda inaagiza kusitisha ufikiwaji na utumiaji, wa moja kwa moja au kinyume chake, kwa mitandao yote ya kijamii pamoja na programu za kutuma ujumbe mitandaoni hadi siku isiyojulikana," Barua kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa tume imesema hivyo kwa watoaji huduma za mtandao.

Msemaji wa tume hiyo Ibrahim Bbossa na msemaji wa serikali Ofwono Opondo hawakujibu simu walizokuwa wanapigiwa ili kutoa maoni yao kuhusiana na hilo.

Afisa katika Wizara ya Habari Judith Nabakooba alisema hakuweza kusema chochote kwa wakati huo.

Wagombea wa urais nchini Uganda

CHANZO- BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post