Tanzia : MSANII WA BONGO FLEVA CPWAA AFARIKI DUNIA

Msanii Cpwaa enzi za uhai wake 
Msanii wa Bongo Fleva Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa'amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 17,2021 akiendelea na matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam ambako alipelekwa kupata matibabu baada ya kuzidiwa ghafla.

Ndugu yake wa karibu Murad Omary, amesema kuwa msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Nimonia.

'Cpwaa alilazwa Muhimbili ICU tangu Jumatano ambapo alikuwa anasumbuliwa na tatizo la Nimonia na usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba au saa nane hivi tukapigiwa simu kutoka Muhimbili kuwa amefariki dunia'', amesema Murad Omary.

Aidha Murad Omary amesema msiba upo Magomeni kwa mama yake mzazi na CPwaa na mazishi yanafanyika leo saa 10:00 jioni kama hakutakuwa na mabadiliko ya ratiba iliyopangwa baada ya kikao cha familia.

CPWAA ambaye aliwahi kuunda kundi la Park Lane akiwa na msanii mwenzake Suma Lee kabla ya kundi hilo kuvunjika mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Hizi hapa baadhi ya nyimbo zake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments