DC KENNAN AZINDUA TAMASHA LA KAN..ASEMA UHURU WA WASANII, KUJIELEZA NA UBUNIFU, HAVIPASWI KUZUIWA


Mkuu wa wilaya ya Arusha Kennan Kiongosi akiongea na mkurugenzi wa Tamasha la KANFESTIVAL Khalifa Mbowe wakati akifungua Tamasha hilo
Mkurugenzi wa Tamasha la Kan Festival Khalifa Mbowe akiongea katika uzinduzi wa Tamasha hilo linalofanyika katika viwanja vya chuo cha Maendeleo na uhusiano wa kimataifa (Ms-TCDC) kilichopo ndani ya Wilaya ya Arumeru.
Makamu mkuu wa chuo Cha MS-TCDC Sara Teri akiongea katika uzinduzi wa Tamasha hilo hii leo (Picha na Woinde Shizza, ARUSHA)
washiriki wa Tamasha la Kan wakifanya mazoezi ya asubuhi.


Na Woinde Shizza , Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi amesema kuwa uhuru wa wasanii na haki ya kujieleza na ubunifu haipaswi kuzuiliwa japo wanatambuliwa kwa kazi zao wanazozifanya.

Aliyasema hayo leo wakati akifungua Tamasha la maarifa, sanaa na kujenga mtandao (KANFESTIVAL) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha, lililoanza leo katika Chuo cha Maendeleo na ushirikiano wa kimataifa (MS-TCDC) ambapo amesema kuwa uhuru wa ubunifu na uhuru wa kujieleza sio kitu pekee kinachowatafsiri wao kama wasanii ila utambuliwa kwa kazi zao lakini uhuru wa kujieleza na kuwa wabunifu ni muhimu.

Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kuunga mkono maonesho na matamsha yanayohusisha wasanii na kazi zetu za utamaduni kwani matokeo ya muziki uwafikia mamilioni ya watu ulimwenguni.

"Tunahakikisha tunaendelea kuisaidia sekta hii muhimu ya uchumi na kukaribisha ushirikiano ambao utaimarisha sekata hii kwa maendeleo ya taifa zetu,"alisema Kenan.

Alieleza kuwa wanapojadili, kulumbana, kuimba na kutazama maonesho ya Kan kwa siku hizo tatu wajikite katika kuelekeza juhudi za maendeleo.

Mkurugenzi wa Tamasha hilo kwa mwaka huu wa 2021 Khalila Mbowe alisema kuwa tamasha la Kan linawasaidia wananchi kujisikia kuwa wao ni sehemu ya maendeleo ya nchi zao kwa kujiona wao ni fursa ya ndiyo majawabu ya kusukuma gurudumu la maendeo ya Afrika.

Alieleza kuwa tamasha hilo litahudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki kutoka nchi za Afrika Mashariki akiwemo G nako, Nikki wa pili Nazizi Grece Matata, Tarajazz Richie, Worriors from the East na Dj Skadi ambapo limeanza January 28 na kuhitimishwa Januari 30 huku asilimia 85 ya tamasha hilo likifanyika mtandaoni kutokana na changamoto ya Corona inayoendelea kuikabili dunia hivi sasa.

Mkurugenzi wa KAN, Khalila Mbowe kwa mwaka huu kuna utofauti mkubwa ambao ni tamasha kufanyika kwa asilimia kubwa mtandaoni, mijadala, kuboresha afya kwa kuwa na mbio maarufu Kan run, pamoja na Kan harcks.

Alisema lengo lao ni kujimuisha bara zima la Afrika bado ndio maana wote ambao ni marafiki wa maendeleo ya afrika wanashiriki Kan Festival kupitia mijadala itayoendeshwa katika mitandao ya kijamii na kuona ni jinsi gani wanaweza kukuza maendeleo ya bara la Afrika hasa kwa kuangalia agenda ya 2063 ya umoja wa mataifa.

“Kusudi la Kan Festival na huu ni mwaka wa tatu na inaendelea kukua na kuonekana ulimwenguni na kwa mwaka huu kutakuwa na mijadala tofauti tofauti hapa na kwenye Mitandao pia na lengo ni moja kuhakikisha tunapotoka hapa tunasemaje au tunatokaje Kama washiriki wa mjadala,” alisema Sara Teri.

Alifafanua kuwa mara nyingi watu wa kawaida wanakosa fursa ya kujadili maendeleo ya bara lao na badala yake kuna kuwa na watu wanaojadili bila sauti za watu wa kawaida kusikika zikionyesa jinsi wanavyoshiriki au kuhusika hivyo lengo ni wewe na yeye mnasemaje juu ya maendeleo ya bara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post