WANAFUNZI 10 BORA , SHULE 10 BORA KITAIFA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2020

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne huku wavulana wakiongoza katika orodha ya wanafunzi 10 bora.

Katika orodha ya wanafunzi 10 bora, wavulana wapo saba na wasichana watatu.

Matokeo hayo yametangazwa leo Ijumaa Januari 15, 2021 na katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.

Shule ya sekondari Cannosa ndiyo iliyong'ara zaidi kwa kuingiza wanafunzi watatu kwenye 10 bora.

Kulingana na orodha hiyo, Paul Luziga wa Panda Hill ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na msichana Justina Gerald wa Canossa.

Mwanafunzi wa tatu ni Timothy Segu wa (Mzumbe), Isaya Rukamya(Feza Boys), Ashraf Ally (Ilboru), Samson Mwakabage (Jude), Derick Mushi (Ilboru).

Wengine walioingia kumi bora ni Layla Atokwete (Canossa), Innocent Joseph (Mzumbe) na nafasi ya 10 ikishikwa na Lunargrace Celestine wa Canossa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post