WMA WATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI KWENYE MAONESHO YA 5 YA BIDHAA ZA VIWANDA

 

Meneja wa Mawasiliano kwa Umma WMA, Bi.Irene John akiwaelekeza wajasiriamali ni namna gani vifungashio vinatakiwa kuwa bora na kumvutia mnunuzi wa bidhaa.

 

Maafisa kutoka WMA wakikagua bidhaa na kuwaelimisha wajasiriamali kuhusu namna ya kuweza kutengeneza vifungashio bora vyenye kufuata taratibu ili kuweza kuinua biashara ya bidhaa hiyo. 

Maafisa wa WMA wakikagua mafuta ya kupikia kwa mmoja wa wajasiriamali walioweza kujitokeza katika Maonesho ya % ya bidhaa za Viwanda yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.


NA EMMANUEL MBATILO

Wakala wa Vipimo (WMA) wametumia maonesho ya 5 ya Bidhaa za Viwanda kwa kutoa elimu kuhusu vipimo kwenye vifungashio vya bidhaa kwa wajasiriamali waliweza kujitokeza katika maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Maonesho hayo Meneja wa Mwasiliano kwa Umma WMA, Bi.Irene John amesema wameamua kutoa elimu hiyo kwa Wajasiriamali wadogo ili waweze kukuza biashara zao na ziweze kujulikana hata nje ya nchi.

Aidha Bi.Irene amesema katika vifungashio, wajasiriamali wameelezwa kuwa lazima watambulishe majina ya biashara mahali wanapofanyia biashara, kiasi halisi kilichofungashwa (baada ya kupima kwa kutumia vipimo sahihi vilivyohakikiwa na Wakala wa Vipimo.

"Katika Vifungashio kunatakiwa kuwepo walau lugha moja ya kiofisi ya nchi bidhaa inakopelekea ndo itumike kuandika kwenye lebo pamoja na kufuata utaratibu sahihi wa uandishi. Mfano.20 kg ndo sahihi na sio 20KG". Amesema Bi.Irene.

Pamoja na hayo Wakala wa Vipimo katika majukumu yake, inafanya uhakiki wa vipimo katika maeneo mbalimbali ya biashara kama maduka ya kuuzia nyama, Viwandani, mizani inayotumika kuuzia bidhaa masokoni ikiwemo bidhaa zilizofungashwa ili kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha inayotolewa.

Vilevile Wakala wa Vipimo inafanya uhakiki wa mizani zote zinazotumika wakati wa ununuzi wa mazao mbalimbali kama zao la pamba, korosho na ufuta.

Hata hivyo kupitia kituo cha kisasa cha upimaji katika eneo la Misugusugu na ofisi za mikoa Wakala wa Vipimo inafanya uhakiki wa dira za maji ambapo mamlaka zote za maji na waagizaji wote huleta dira zao kwa ajili ya kuhakikiwa.

Pia Wakala wa Vipimo inafanya uhakiki wa mizani zinazotumika kwenye vituo vya afya ili kutoa uzito sahihi wa wagonjwa na watoto mara wanapozaliwa .

Mbali na hayo Wakala wa Vipimo inahakiki traffic Speed radar (tochi) zinazotumiwa na maaskari barabarani ili ziweze kutoa vipimo sahihi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post