WAZIRI UMMY :TUTAWACHUKULIA HATUA KALI WENYE VIWANDA VINAVYOTIRIRISHA MAJI TAKA YENYE SUMU.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa Jiji la Tanga kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim,Mkurugenzi wa Jiji hilo Daudi Mayeji na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa Jiji la Tanga kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim,Mkurugenzi wa Jiji hilo Daudi Mayeji na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba
Mshtahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Abdurahamani Shiloo akizungumza wakati wa kikao hicho
WAZIRI nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (MB) Ummy Mwalimu katikati akila kiapo cha udiwani Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya wilaya  ya Tanga Luth Mkisi wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani leo kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge kulia ni Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CCM) Abdurahmani Shiloo
Meze kuu wakifuatilia matukio mbalimblai kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanasha Ulenge akifuatiiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM),Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salimu ,Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakifiatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Abdurahamani Shiloo kushoto akiwa na Naibu Meya Jiji hilo Joseph Colvas
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakiwa kwenye kikao wakifuatilia matukio mbalimbali

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakiwa kwenye kikao wakifuatilia matukio mbalimbali

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu amesema atawachukulia hatua kali za kisheria wenye viwanda ambavyo vinatiririsha maji taka yenye sumu yanayochangia uchafuzi wa  mazingira.

Kauli hiyo aliitoa leo wakati akizungumza katika kikao cha kuwaapisha madiwani wa Halimashauri ya Jiji la Tanga kilichofanyika katika ukumbi wa halimashauri ya Jiji hilo alisema kuwa atahakikisha anasimamia kwa ukaribu sheria ya utunzaji wa mazingira.

Alisema kuwa hatafumbia macho iwapo itabainika kuna kiwanda hapa ambacho kinatiririsha maji taka yenye sumu kwa makusudi katika makazi ya watu au kwenye mifereji kinyume na maelekezo ya waliyopewa ya udhibiti wa maji tiririka

“Nitahakikisha nakula nao sambamba wenye viwanda ambao bado mpaka sasa wanaendelea kutuchafulia mazingira yetu licha ya maelekezo ambayo tayari serikali ilikwisha kuyatoa ya kuhakikisha wanayatibu maji hayo kabla ya kuanza kuyamwaga kwenye mitaro”alisema Waziri Ummi.

Aidha alizitaka halimashauri zote nchini kuhakikia wanahasisha wananchi kwenye maeneo yao kujenga tabia ya upandaji wa miti ili kudhibiti mabadiliko ya tabia nchini yanayotokana na kuzalisha hewa ukaa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobiasi Mwilapwa akitoa salamu za wilaya hiyo alisema kuwa elimu bure imesababisha uhaba wa miundombinu ya madarasa katika shule zilizoko wilayani humo.

Alisema kuwa hali imesababisha wilaya hiyo kukumbwa na uhaba wa madarasa 44 kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza kutokana na ongezeko la kiwango cha ufaulu katika mitihani yao ya darasa la saba.

“Kwa mwaka jana matokeo ya ufaulu wa darasa la saba yameongezeka kwa asilimia 87% hivyo kupelekea uhaba wa vyumba vya madarasa kwa wananfunxzi wanokwenda kidato cha kwanza”alisema DC Mwilapwa.

Aidha Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo aliwakumbusaha madiwani kuwa wanadeni kubwa kwa wananchi wa jiji hilo la kuwaletea maendeleo na utatuzi wa kero zilizoko kwenye maeneo yao.

“Tunajukumu la kuwasaidia wananchi kusimamia maendeleo lakini ni kuwatafutia ufumbuzi wa kero zao ,niwatake mwende mkawe sehemu ya majibu ya kero zao badala ya kuwa watazamaji tuu bila kuchukuwa hatua stahiki”alisema Meya Shiloo.

Nae Katibu Tawala wa Jiji la Tanga Faidha Salimu aliwataka madiwani kwenda kuwa walinzi wa amani kwenye maeneo yao kutokana na kuibuka kwa viashiria vya uvunjifu wa amani ikiwemo vitendo vya ukabaji na wizi.

“Niwaombe mwende mkawe mabalozi wa kuhamasisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yenu kwani tayari tunataarifa za uwepo wa vikundi vya watu ambavyo vimeanza kutishia hali ya usalama kwenye maeneo yetu,hivyo kupitia nyie mtaweza kubadilisha hiyo hali”alibainisha DAS Salim.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments