WATENDAJI WA KATA NA MAAFISA KATA WA BUKOBA MANISPAA WAPATA ELIMU YA LISHE BORA

Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (Mb)akizungumza wakati akitoa elimu ya  Lishe kwa Watendaji wa Kata, Maafisa Kata wa Maendeleo ya Jamii, Afya, Kilimo n.k. kutoka Bukoba Manispaa.

Sehemu ya Watendaji wa Kata, Maafisa Kata wa Maendeleo ya Jamii, Afya, Kilimo n.k. kutoka Bukoba Manispaa wakifuatilia kwa umakini elimu ya Lishe

Shirika la Agri Thamani limetoa Elimu ya Lishe kwa Watendaji wa Kata, Maafisa Kata wa Maendeleo ya Jamii, Afya, Kilimo n.k. kutoka Bukoba Manispaa.
 
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (Mb) alisema kuwa masuala ya lishe ni mtambuka hivyo ni muhimu kuhakikisha Viongozi na Watendaji wote wanaongea lugha moja.
 
Alisema kwa kufanya hivyo kama Taifa tunaweza kufikia malengo tuliyojiwekea ya kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa ujumla. 

Aidha alisema watendaji na maafisa 57 wamenufaika na mafunzo haya na wameahidi kuibeba Ajenda ya Lishe Bora kwenye maeneo yao. 

Mbunge Lugangira alisisitiza kuwa hatua inayofuata ni kushuka chini kata moja baada ya nyingine hadi kuhakikisha  kwamba Lishe Bora inakuwa kwa vitendo.

Kazi hii itafanyika kwa kushirikiana kwa karibu na Watendaji Kata na Maafisa Kata na ndio msingi wa kuwafikishia semina hii alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments