MHANDISI MAGANGA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU WA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)

DODOMA:

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) katika kikao kilichofanyika Desemba 20, 2020 imemteua Mhandisi Amos William Maganga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuanzia tarehe 16 Desemba 2020 kwa mujibu wa kifungu cha 25(1) cha Sheria Namba 8 ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005.

Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Maganga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA. Mhandisi Maganga ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya nishati. Aidha, ameshika nyadhifa mbalimbali toka alipokua ameajiriwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Bodi inaomba ushirikiano kutoka kwa wadau wote ili kumuwezesha Mhandisi Maganga kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wakala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments