MAHAKAMA YA MAFISADI YAAHIRISHA HUKUMU YA AYUB KIBOKO NA MKEWE
Monday, December 14, 2020
Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Ayubu Kiboko na Mkewe Pilly Mohamed hadi Desemba 18 mwaka huu.
Uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo umetolewa na Msajili wa mahakama hiyo David Ngunyale baada ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi yao iliyotarajiwa kutolewa leo baada ya upande wa mashtaka kufunga jalada la ushahidi lililokuwa na mashahidi 16.
Katika Kesi ya msingi namba 29/2018, Kiboko na mkewe wanadaiwa kukamatwa Mei 23 mwaka 2018 eneo la Tegeta Nyuki – Masaiti wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakiwa wanasafirisha dawa za kuĺevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 251.25 kinyume na sheria.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin