MWANAMKE AIBA MTOTO KANISANI ILI KULINDA NDOA YAKE


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu
**
Lilian Stanley (36) mkazi wa Tumbaku, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma ya wizi wa mtoto wa mwezi mmoja katika kanisa la Ufufuo na Uzima Lililopo kata ya Mkundi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 22, 2020, na Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu, amesema kuwa tukio hilo limetokea Desemba 6, 2020, majira ya saa 4:00 asubuhi.

Kamanda Muslimu ameongeza kuwa wakati tukio hilo linatokea mama mzazi wa mtoto huyo Neema Selemani (27), aliomba msaada wa kushikiwa mtoto wake na mtuhumiwa huyo lakini baada ya muda mfupi alitoweka pasipo kujulikana ambapo uchunguzi wa awali ulibaini mtuhumiwa alifanya kitendo hicho ili kulinda ndoa yake.

"Desemba 19, 2020, tulimkamata Lilian akiwa na mtoto huyo, mbinu alizozitumia kuiba huyo mtoto kwanza alifanya urafiki na huyu mama tangu akiwa mjamzito, wakawa wanakwenda wote kanisani na baada ya kujifungua kwa kuwa alimuamini akamuachia huyo mtoto na kutoweka naye, lakini sababu kubwa ni kulinda ndoa yake ili amdanganye mumewe kama amejifungua", amesema Kamanda Musilimu.

CHANZO- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments