WAZIRI KALEMANI AFANYA ZIARA MGODI WA NYANGALATA KAHAMA....AAGIZA KASI YA USAMBAZAJI UMEME


Waziri wa Nishati Dkr Medard Kaleman, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhuru wilayani Kahama, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu

Na Marco Maduhu -Kahama. 
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga, ambapo leo ametembelea Mgodi mdogo wa uchimbaji madini ya dhahabu Nyangalata uliopo Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama. 

Akiwa katika mgodi huo, akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu, Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha, pamoja na maofisa kutoka Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), Dk. Kalemani amesema Serikali inataka kasi ya usambazaji umeme kwenye migodi midogo ya madini ili kuondoa gharama kubwa za uzalishaji wa madini hayo. 

Amesema kwenye migodi midogo ya uchimbaji wa madini ya dhahabu, hua wanatumia gharama kubwa ya uzalishaji wa madini hayo kutokana na kutumia mafuta mazito ama Jenereta, lakini wakitumia Nishati ya umeme kutoka Gridi ya Taifa hawatakuwa wakiingia kwenye gharama hizo kubwa kama ilivyo sasa. 

“Rais John Magufuli ameshatoa fedha ili wananchi wasambaziwe huduma ya umeme yakiwamo na maeneo ya migodi midogo, hivyo naagiza Januari 3, 2021, watu wa Survey wawe wameshafika kwenye eneo hili la mgodi wa Nyangalata na kuanza mchakato wa kuleta huduma ya umeme hapa, pamoja na kwenye mgodi wa Tambarare,” amesema Dk. Kalemani. 

“Lengo la Rais Magufuli ni kuwakuza wachimbaji wadogo, ili wachimbe madini kwa ufanisi, na kuongeza kasi ya uzalishaji wa madini na kupata mapato mengi, na hatimaye kukua kiuchumi na taifa kwa ujumla, na mkitumia umeme mtaokoa gharama ya asilimia 80 ya uzalishaji madini ambayo mnaingia kwa sasa na kutumia Shilingi Milioni 800 kwa mwezi,”ameongeza. 

Pia amesema Serikali hadi kufikia Februari 5, mwaka 2021, wanatarajia kuanza kusambaza pia huduma ya Nishati ya umeme kwenye vitongoji na vijiji vyote nchi nzima, ambapo katika wilaya ya Kahama vimesalia vijiji 147, na Halmashauri ya Msalala kuna vijiji 60. 

Katika hatua Nyingine Waziri Kalemani, akiwa katika kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza (Substation) kilichopo Bulyanhulu wilayani Kahama, ambacho kinapokea umeme kutoka Ibadakuli mjini Shinyanga, amekazia suala kukata umeme hovyo hasa katika Sikukuu ya Mwaka Mpya, na kuonya umeme huo usije ukathubutu kukatika hata kidogo Mkoani Geita wala kushtua, ambapo kwa sasa Rais yupo kwenye mapumziko ya Sikukuu hiyo nyumbani kwake Chato. 

Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu, amesema kasi hiyo ya usambazaji umeme kwenye makazi ya watu na maeneo ya migodi, itakuwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa maendeleo kwa wananchi pamoja na wachimbaji wadogo, ikiwamo na kufungua vitega uchumi vya umeme na kuwaongezea kipato. 

Kwa upande wake mmoja wa wachimbaji wadogo kutoka mgodi huo wa Nyangalata Alex Manyama, amesema kutokana na kutumia mafuta mazito kuzalisha madini hayo, amekuwa akitumia kwa siku kiasi cha Shilingi Laki Tisa, na kuomba Serikali iwapelekee huduma hiyo ya Nishati ya umeme, ili kuwapunguzia matumizi hayo ya gharama kubwa. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Mgodi wa Nyangalata na kuwahakikishia kuwa Serikali itawaletea umeme ili kuwapunguzia gharama kubwa za uzalishaji madini kwa njia ya mafuta mazito na Jenereta.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kasimu akizungumza na wachimbaji wadogo Nyangalata.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha, akizungumza na wachimbaji wadogo Nyangalata.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, akizungumza na wachimbaji wadogo wa Nyangalata.
Wachimbaji wadogo wa madini Nyangalata wakiwa kwenye mkutano wa Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani.
Wachimbaji wadogo wa madini Nyangalata wakiwa kwenye mkutano wa Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, akiangalia namna ya uzalishaji madini ya dhahabu kwa wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Nyangalata, kwa kutumia Jenereta ambapo wanaingia gharama kubwa.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, kushoto, akisikiliza maelezo kwa mchimbaji mdogo Alex Manyama namna wanavyotumia gharama kubwa kuzalisha madini ya dhahabu kwa njia ya mafuta mazito au Jenereta.
Wachimbaji wadogo wakiwa kwenye shughuli za uchenjuaji madini.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhulu wilayani Kahama, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu
Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhulu wilayani Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Annamringfi Macha kizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhulu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhulu.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa kituo cha kupokea umeme, kusambaza na kupoza kutoka eneo la Bulyanhulu Amos Asheli.
Awali Waziri wa Nishat Dk. Medard Kalemani, akiwa kwenye ziara katika mgodi wa madini Nyangalata.
Ziara ikiendelea.
 

Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.

Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.
 

Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.

Na Marco Maduhu- Kahama.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments