MTENDAJI KOLANDOTO AONGOZA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI UJENZI VYUMBA MADARASA

 

 

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga Mwakaluba Wilson, akiongoza wananchi wa Kata hiyo kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto ili kupungufu upungufu wa madarasa uliopo shuleni hapo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga. 

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga Mwakaluba Wilson, wameongoza wananchi wa Kata hiyo kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kolandoto, ili kupunguza tatizo la upungufu wa madarasa uliopo shuleni hapo.


Akizungumza leo wakati wa uchimbaji wa msingi huo, Wilson amesema wamehamasisha wananchi kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na Serikali, ili kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo ya Kata, na kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma. 

Amesema Shule hiyo ya Sekondari ya Kolandoto ina uhitaji wa vyumba vya madarasa 13, yaliyopo ni saba, na hivyo kuwa na uhitaji wa madarasa sita, ambapo kwa sasa kwa kushirikiana na wananchi wanajenga madarasa mawili, na kufanya shule hiyo kuendelea kukabiliwa na upungufu wa madarasa manne. 

“Sisi kama Serikali tunashukuru sana wananchi kuitikia wito huu, na kujitokeza kwa wingi kuja kuchimba msingi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule hii ya Sekondari Kolandoto, ili kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa uliopo shuleni hapa,”amesema Wilson. 

Naye Diwani wa Kata hiyo ya Kolandoto Mussa Andrew, amesema kitendo walichokifanya wananchi wake kujitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kimemtia moyo sana, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo. 

Nao baadhi ya wananchi wa Kolandoto ambao waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa akiwamo Debora Magoso, wamesema wameamua kuunga juhudi za serikali ili kuhakikisha watoto wao wanasoma katika mazingira mazuri na kutimiza ndoto zao, na kuja kuwa msaada kwao pale watakapo zeeka. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mwakaluba Wilson, akizungumza kwenye zoezi la uchimbaji msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto.
Diwani wa Kata ya Kolandoto Mussa Andrew, akielezea namna alivyoguswa na wananchi kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo kwa kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto.
Mwananchi Debora Magoso, akielezea namna walivyoguswa na kuamua kushirikiana na Serikali kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga Mwakaluba Wilson, akiongoza wananchi wa Kata hiyo kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto ili kupungufu upungufu wa madarasa uliopo shuleni hapo.
Afisa Mtendaji akiendelea kuchimba msingi.
Diwani wa Kata ya Kolandoto Mussa Andrew akichimba msingi kwa kushirikiana na wananchi ili kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto.
Wananchi wa Kolandoto wakichimba msingi kwa ajili ya kushirikiana na Serikali kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto.
Zoezi la uchimbaji msingi likiendelea.
Zoezi la uchimbaji msingi likiendelea.
Zoezi la uchimbaji msingi likiendelea.
Zoezi la uchimbaji msingi likiendelea.
Zoezi la uchimbaji msingi likiendelea.
Wananchi wa Kolandoto wakiwa wamebeba majembe kwa ajili ya kuchimba msingi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post