ABIRIA AFARIKI DUNIA NDANI YA BASI


Abiria mmoja amefariki dunia akiwa ndani ya basi lililokuwa likisafiri kuelekea kaunti ya Machakos kutoka Bungoma nchini Kenya.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 68 alikata roho akiwa eneo la Kibwezi siku ya Jumanne, Disemba 15,2020. 

Wasafiri wenzake walijawa na wasiwasi huku baadhi wakibashiri huenda mwendazake aliangamizwa na virusi vya corona.

 Kulingana na ripoti ya polisi, abiria aliyekuwa ameketi karibu na marehemu alijaribu kumwarifu afunge dirisha lakini hakujibu wala kuonyesha dalili za kuwa hai. 

Akithibitisha kisa hicho, kamanda mkuu wa polisi kata ndogo ya Kibwezi Ben Changulo alisema abiria huyo alifariki dunia baada ya kushindwa kupumua.

 " Basi la sacco ya Kathi lilipokaribia mji wa Kibwezi, ilibainika kwamba abiria mmoja alikuwa ameaga dunia, abiria aliyekuwa ameketi karibu naye alimtaka afunge dirisha lakini hakuwa akizungumza," Changulo alisema.

 Kisa hiki kinajiri takribani mwezi mmoja baada ya abiria mwingine kufariki dunia akiwa ndani ya matatu katika barabara kuu ya Mombasa.

 Abiria huyo alikata roho Ijumaa, Novemba 27 akiwa katika mji wa Malili. Kulingana nakamishna wa kaunti ya Makueni Maalimu Mohammeed, basi alimokuwa akisafiria abiria huyo lilikuwa linatokea kaunti ya Bungoma na lilikuwa limewabea abiria 32.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post