EWURA NA LATRA WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KUPUNGUZA MLOLONGO WA HUDUMA ZAO KWA WATEJA

 


NA EMMANUEL MBATILO

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (ewura) kwa kushirikiana na Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) Wametilina saini hii leo mkataba maaalumu wa mashirikiano wenye lengo la kupunguza mlolongo wa huduma zao kwa wateja.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa bodi ya Ewura Ahmad Kilima amesema mkataba huo utakuwa chachu ya kuboresha huduma na kuondoa usumbufu kwa wateja wa kuzunguka katika kila ofisi ya mamlaka hizo.

Ameongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mamlaka na taasisi mbalimbali za serikali kuungana na kushirikiana katika utoaji wa huduma zao ili kuweza kufika mbali na kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuongeza uaminifu kwa wadau.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Latra Gillard Ngewe amesema watahakikisha wanaongeza udhibiti wa magari mabovu yanayobeba mnafuta ili kupuondoa changamoto ya uchakachuaji mafuta njiani.

Aidha mkataba huo wa malidhiano ya mashirikiano ni ya msingi kwa mstakabali wa uchumi wa Taifa, kutokana na nchi za ukanda wa afrika mashariki na SADC wanategemea Tanzania kuwasambazia mafuta.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post